Ole Sabaya Aagiza Kukamatwa Wamiliki wa Mabasi Kwa Kuhujumu Miundombinu ya Reli






Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameagiza wamiliki wawili wa mabasi kukamatwa kwa tuhuma za kuunda Genge la Uhalifu kwa lengo la kuhujumu miundombinu ya reli ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam- Moshi

Sabaya amesema, magenge ya watu hayo walionekana wakilegeza nati, wakiweka mawe makubwa katikati ya reli au kuchimba mashimo ili kuwe na matatizo katika Usafiri wa Treni

Wafanyabiashara hao waliotakiwa kuripoti kituo cha Polisi Bomang'ombe jana Jumapili Januari 19, 2020 kabla ya saa 10 jioni ni Clemence Mbowe anayemiliki mabasi ya Machame Safari na Rodrick Uronu wa mabasi ya Lim Safari

Clemence Mbowe amesema kuwa, tuhuma hizo za yeye kuhujumu siyo za kweli na kwamba yeye yupo Dar es salaam na ameona kwenye Mitandao ya Kijamii hivyo ataenda Moshi na kufika Ofisini kwa Sabaya kutaka kujua tuhuma hizo -
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad