Papa Benedict Amuonya Papa Francis Kuhusu Ndoa za Makasisi
0
January 13, 2020
Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 ametetea suala la makasisi kutofunga ndoa wakati ambapo mrithi wake anafikiria kulegeza marufuku hiyo kwa wanaume wanaooa ambao wanahudumu kama makasisi.
Papa Benedict amesema hayo katika kitabu walichoshirikiana na Kadinali Robert Sarah.
Hatua hiyo inawadia kujibu pendekezo la kuruhusu wanaume waliooa kutawazwa kama makasisi katika eneo la Amazon.
Papa Benedict, ambaye alistaafu mwaka 2013, amesema hakuweza kunyamazia suala hilo.
Katika kitabu hicho, Papa Benedict amesema kutofunga ndoa kwa makasisi ni utamaduni wa kale ambao umekuwepo kwa karne nyingi tu ndani ya kanisa hilo, una umuhimu mkubwa kwasababu unaruhusu makasisi kuangazia majukumu yao.
Papa Benedict mwenye umri wa miaka 92 amesema "Halionekani kuwa jambo linalowezekano kutimiza majukumu ya ukasisi na ndoa kwa wakati mmoja".
Ni nadra sana kwa Papa Benedict ambaye alikuwa wa askofu wa kwanza kujiuzulu katika kipindi cha karibia miaka 600, kuingilia masuala ya ukasisi.
Vatican bado haijasema lolote kuhusu na kitabu hicho, ambacho kiliangaziwa kidogo katika gazeti la Ufaransa la Le Figaro kabla ya kuchapishwa leo Jumatatu.
Wachambuzi wa Vatican wameshangazwa na hatua ya Papa Benedict kuingilia suala hilo, na kuongeza kwamba hatua ya Papa Benedict inavunja utamaduni ambao umekuwepo.
"Papa Benedict siyo kwamba anavunja ukimya wake kwasababu hakuhisi kwamba anavunja ahadi kwa kiapo alichokula. isipokuwa amekiuka kabisa,"Massimo Faggioli, mwanahistoria na mwanatheolojia. katika chuo kikuu cha Villanova ameandika katika mtandao wa Twitter.
Mwanathiolojia mwenye msimamo mkali ambaye anashikilia mtazamo wa tangu jadi na maadili ya kanisa amesema, Papa Benedict aliahidi kusalia kimya wakati anastaafu, akitaja hali mbaya ya afya.
Lakini tangu wakati huo, amekuwa akitoa maoni yake kupitia Makala, vitabu na mahojiano, akitaka papa Francis kuchukua njia tofauti, ambaye anaonekana kupendelea mabadiliko. Papa Benedict bado anaishi Vatican katika yaliyokuwa makao ya watawa.
Tags