Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole amemtolea uvuvi Zitto Kable kwa kitendo cha kuzuia fedha za elimu huku akimuambia watashinda Uchaguzi Mkuu hata akizuia fedha hizo.
Zitto ambaye ni kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo aliandika barua za kutaka Benki ya Dunia kusitisha mkopo wa elimu baada ya kudai serikali inakiuka taratibu huku ikizui wanafunzi waliopata ujauzito wasiendelee na masomo.
Pia zitto alisema mkopo huo sio kweli ulilenga kuwanufaisha wanafunzi na kwamba ni kwa ajili ya kampeni za kisiasa.
Polepole baada ya kuona taarifa hiyo alimjibu kuwa
“Kumbe tatizo ni Uchaguzi 2020. Kabwe anaomba tunyimwe mkopo wa kuongeza udhubutu wa elimu ya watoto wetu kwa sababu anajua ni jukumu letu kujenga shule na sifa zitakuja CCM,” aliandika polepole.
Aliongezea kuwa
” Inayokwama sio CCM ni watoto wa Kigoma Ujiji. Kushinda tutashinda tu! Najiuliza watoto wake wanasoma wapi?,”