Rais Magufuli Atoa onyo kwa Viongozi wa CCM Kuelekea Uchaguzi Mkuu.....Asema ATCL Sasa Kupaa China Moja kwa Moja



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Rais John Magufuli amewataka viongozi wa mikoa wa chama hicho kutokuwa na majina yao mfukoni katika  mchakato wa kura maoni kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020  jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi wa mikoa, wilaya na jumuiya za chama hicho kutoka mikoa yote nchini.

“Nawashukuru sana wajumbe, kwa kweli leo nina raha sana, na kama ndugu Bashiru unafikiri lolote baya leo hakuna baya shetani ameshindwa. Leo ni siku ya raha ya kukutana na Chama kikubwa kilichoshika hatamu ya uongozi wa Taifa hili.

“Niliona tukutane hapa kwanza tukishamaliza hapa tutakwenda Ikulu kupiga picha na kama kuna maji tutakunywa wote pamoja, Ikulu ni yenu na ninyi ndiyo mlinipeleka Ikulu ahsanteni sana.

“Eneo la fedha na uchumi tumeweza kuchukua hatua mbalimbali kuhakiki, kurejesha na kuthaminisha upya mali na rasilimali za Chama, na jitihada hizo zimeongeza mapato kutoka Tsh Bil 46.1 hadi mwaka 2015/16 hadi tsh Bil 59.8 mwaka 2018/19.

“Baada ya tathimini na shughuli ya uhakiki wa mali za Chama, thamani yake imepanda kutoka Bilioni 41.033 Mwaka 2016/2017 na kufikia Bilioni 974.66 mwaka 2020, ongezeko la asilimia 2275.3%. Tathmini hii ni ya mikoa13 tu na kazi bado inaendelea.

“Niwaombe Viongozi wenzangu ndani ya Wilaya na Mikoa wakati wa mchakato wa uchaguzi tusiende na majina mfukoni tuoneshe ukomavu mwaka huu, tuwaache wengine wakurupuke kuvunja taratibu wagombane, tusikate majina ya Wagombea kwasababu zetu binafsi

“Mtu unajijua ni Mchezaji mzuri unaficha chenga zako kwanini?, tujiandae na uchaguzi, CCM hii sio ile ya nyuma na Wapinzani wetu sio wale wa nyuma, Wapinzani wamebadilisha mikakati yao, mingine wanaiweka hadharani na mingine ni ya kificho, tusibweteke

“Fedha zilizopo sasa hivi tuna uwezo wa kuendesha nchi kwa miezi 6, hatakama tusipokusanya leo hela tunaweza kuendesha nchi kwa miezi 6 ndiyo maana tunapata fedha za kujenga miradi mikubwa.

“Wala pasitokee Kiongozi yoyote ndani ya Serikali atakaye sema Chama kinanifatafata, lazima Chama kikufate kama hutaki kufatwa ondoka upishe tuweke watu wengine.

“Hatutaki Chama hiki kuwa ombaomba ambacho kinategemea matajiri ambao baadae wamekuwa wakikiweka Chama mfukoni. Serikali iliyopo madarakani leo ni ya CCM. Viongozi niliyowateuwa wote, ujue unakwenda kutekeleza masuala ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

“Watendaji wa serikali nataka kutoa wito na Waziri Mkuu uko hapa, wasisitizeni viongozi wa serikali walioko madarakani chama lazima kitawafuata, chama lazima kiangalie matokeo halisi ya miradi inayotekelezwa kule.

“Tuliomba mikopo hawakutupa, tukabana fedha za mafisadi tukajenga wenyewe, huu mradi wa umeme ndugu zangu umepigwa vita sana lakini ulikuwa unapigwa vita kwa sababu watu walikuwa wana interest ya Selou.

“Idadi ya Watalii wameongezeka kutoka Mil. 1.1 mwaka jana hadi zaidi ya Mil. 1.5, tunataka tujenge uchumi wa nchi iliyo tofauti, lakini hata kuzaana hatuko nyuma, kuzaa ni uchumi msidanganywe.

“Mwezi Februari Tanzania itaanza Safari za Ndege kutoka Nchini kwenda China moja kwa moja. Ndege nyingine zinakuja na tumenunua kwa fedha taslimu. Tajiri huwezi kununua kwa kukopa,” amesema Rais Magufuli. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad