Rais Museveni Atembea Msituni Kukumbuka Vita ya Ukombozi


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni jana alianza ziara ya siku sita msituni kupitia njia aliyotumia katika vita kabla ya kuchukua Serikali kwa njia ya mapinduzi miongo mitatu iliyopita.

Ameanza kutambea kilometa 195 kutoka Galamba kaskazini mwa kampala, ziara itakayokamilika januari 10 katika eneo la Birembo, kusini mwa jiji hilo eneo ambalo majeshi yake alikabiliwa na upinzani mkali kabla ya kuangusha Serikali ya Obote.

“Safari hii muhimu imeanza leo na itachukua siku sita, hii safari ambayo Rais anaongoza ni kumbukumbu ya mambo yaliyopita ili kufurahia yaliyopo” amesema ofisa habari mwandamizi wa Rais Museveni.

Ziara hiyo imekuja baada ya mwezi mmoja tangu Rais huyo afanye matembezi mengine katika Jiji la Kampala ya kupiga vita ufisadi.

Museveni ni miongoni mwa marais wa muda mrefu barani Afrika aliyechukua madaraka mwaka 1986 baada ya kuongoza vita ya msituni dhidi ya utawala wa Idi Amini na Milton Obote, na anatarajiwa kuomba awamu ya sita katika uchaguzi ujao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad