Rais wa Iraq Akutana na DONALD Trump Huko Davos


Taarifa kutoka afisi ya rais wa Iraq inasema Rais wa nchi hiyo Barham Salih amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump huko Davos, Uswisi leo.

Mkutano huo ndio wa kwanza kati ya marais hao wawili tangu Marekani kumuua kamanda wa ngazi ya juu wa Iran Qasseim Soleimani.

Trump ambaye anatarajiwa kuondoka huko Davos leo na kurudi Washington amesema kuna mengi muhimu watakayoyajadili.

Rais Salih naye amesema kukutana na Rais Trump ni fursa muhimu sana.O Ton Salih"Tumekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Marekani imekuwa mshirika wa Iraq na vita dhidi ya kundi la ISIS.

Mpango huu unastahili kukamilishwa. Naamini kwamba mimi na wewe tuna maono sawa ya Iraq iliyo imara, huru ambayo ina amani pamoja na majirani zake."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad