Roma Asimulia Alivyopambana Kunusuru ndoa ya Stamina


Baada ya Stamina kuachia video ya wimbo wake mpya unaohusisha story ya maisha yake ya ndoa, mtu wake wa karibu na msanii mwenzake Roma Mkatoliki ambaye pia alikuwa msimamizi wa harusi yake amefunguka kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM na kuelezea ilivyokuwa mpaka ndoa hiyo ikavunjika.

Roma amesema inakaribia mwaka sasa toka mke wa Stamina alivyoondoka nyumbani kwa mumewe huku yeye na mke wake wakiwa wameshashiriki mara kadhaa kuwapatanisha Stamina na mkewe lakini ikashindikana.

''Huo wimbo kila kitu ni story ya kweli ila mimi kama msimamizi wake na mlezi wake wa ndoa nimejaribu kuweka sawa kwa kuweka vikao vingi kusuluhisha  ila ilifika mahali nimeshindwa ila mkewe aliondoka toka march mwaka jana kutokana na migogoro ya ndoa kama ilivyokua kwa ndoa nyingine'' alisema Roma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad