Serikali Kuzuia Uagizwaji wa Carbon Dioxide

 
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amesema kuwa Serikali imeunda timu maalumu kwa ajili ya kufanya tathmini ya kujua mahitaji ya ndani na uwezo wa uzalishaji wa gesi ya Carbon dioxide na kwamba itakapojiridhisha itapiga marufuku uagizwaji wa gesi hiyo kutoka nje.

Hayo ameyabainisha leo Januari 29, 2020 bungeni Dodoma, katika Mkutano wa 18, Bunge la 11, Kikao cha Pili, wakati akijibu swali la Mbunge wa Busekelo, Fredy Mwakibete, aliyehoji upi ni mpango wa Serikali katika kutoa elimu kwa wananchi, wanaozunguka visima vya gesi ya ukaa na Carbon dioxide ili isiendelee kuleta athari pamoja na kujua ni lini sasa wataanza kuvutia wawekezaji juu ya gesi hiyo.

"Kwa sasa tumeunda timu kwa ajili ya kufanya tathmini kwa muda wa miezi mitatu ili kujua mahitaji ya ndani na tukijiridhisha uwezo wa ndani unao uwezo wa kuzalisha vinywaji kama soda na bia tutazuia kabisa Carbon dioxide kutoka nje" amesema Dkt Kalemani.

Visima vya Gesi ya Ukaa na Carbon dioxide, vinapatikana katika Kijiji cha Mpata ambavyo vimekuwa vikileta athari kwa binadamu, wanyama na mimea wanaozunguka eneo hilo na kwamba Serikali pamoja na wamiliki wa visima hivyo, wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu sahihi kwa wananchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad