SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU VIRUS VYA CORONA NCHINI CHINA




 Serikali imewataka watanzania kuwa watulivu, makini na kupenda kuwa na subira ya kupata maelezo,maelekezo na ufafanuzi rasmi wa Serikali pale kunakotokea jambo badala ya kukimbilia kwenye mitandao na uvumi ili kuondoa kueneza hali ya taharuki kwa wananchi bila ya kuwa na uhakika.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya hali ya Watanzania waishio nchini China kutokana na kuzuka kwa virusi vya homa ya corona nchini humo.

Prof. Kabudi amesema Tanzania ina wanafunzi takribani 4000 ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 na kwamba kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Mbelwa Kairuki ameihakikishia serikali kuwa mpaka sasa hakuna mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.

Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kujua maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni Wuhan na China kwa Ujumla.

Aidha amewataka Watanzania kuwa makini na suala la kutoa taarifa zisizo rasmi ama uvumu kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za Tanzania na kuwataka kuwa na Subira kupata taarifa rasmi kutoka serikalini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad