Shahidi kesi ya vigogo Chadema atoa ushahidi wake



SHAHIDI wa 13, wa upande  wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa,  askari Polisi walimpekua na kumchukulia Sh.2700  na kumuachia Sh. 200 baada ya kumtaka ajiongeze ili waweze kuwmuaachia.

Shahidi huyo ambaye ni Mwanafunzi wa DIT, Lukola Kahumbi amedai hayo leo Januari 24, 2020 Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kuongeza kuwa, kitendo kile kilimsababisha atembee kwa miguu kutoka kituoni  Kinondoni hadi chuoni.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Peter Kibatala kutoa ushahidi wake,  amedai mwaka 2018 alikuwa akisoma Chuo cha DIT akichukua Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano, ambapo kwa sasa anaishi Mbezi Kimara.

Amedai kuwa, alishawahi kuwa Kada wa CCM mwaka 2000 hadi 2014 ambapo aliingia Umoja wa Vijana lakini baadaye akaacha siasa na kuingia Chuo cha DIT.

Amedai, Februari 16,  mwaka 2018 alikuwa katika kituo cha Polisi Oysterbay akiwa katokea chuoni kuelekea kwa shangazi yake Studio Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa aladala ambapo mara baada ya kushuka akiwa kituoni hapo aliona magari ya Polisi mengi huku askari Polisi wakiwa wanashuka kwa kuruka kutoka katika magari hayo jambo ambalo liliibua taharuki na kufanya watu wakimbie akiwemo yeye.

Amedai baada ya kuanza kukimbia, askari waliwakimbiza  na walikamatwa watu mbalimbali wakiwemo wauza vitanda vya chuma wakawekwa katika gari(Difenda) na yeye aliwekwa chini ya siti na wengine wakapandishwa juu na kuchanganywa wanawake na wanaume na kupelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay.

Shahidi huyo, amedai  baada ya kufikishwa kituoni waliwaweka eneo la nje ambapo Askari walitoka ndani na kuanza kuwapiga mikanda, kisha Askari mmoja alitoka na kumpa  ngoma mmoja wao na apige ngoma na wao waanze kuimba ambapo aliyekuwa akiimbisha ni Askari Polisi ambapo kati ya maneno aliyoyasikia ni "Dola si lelemama" kisha Askari aliwaambia anayetaka kukojoa ruhusa ipo na yeye alikuwa mmoja wapo.

"Wakati nikienda chooni, askari wawili walinifuata na kuniambia nijiongoze, huku wakiniuliza kama nilikuwa na chochote skari mmoja akaniuliza kama nina chochote mfukoni ambapo nilikuwa na Elfu 12 na Mia Saba, lakini kabla sijakaa sawa, askari mmoja aliingiza mfukoni na kuchukua sh 2500 lfu 12 na kuniachia 200 kisha wakanambia niodoke nisigeuke nyuma,"

Amedai kuwa hela hiyo aliyobakiwa nayo ilikuwa haitoshi kupanda daladala hivyo akalazimika kurudi Chuo kwa Mguu.

Shahidi huyo aliulizwa alichukua hatua gani baada ya kitendo hicho ambapo amedai alimshirikisha jirani yake yake aitwaye Massawe ambaye ni Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.Pia aliulizwa kama anawakumbuka askari hao lakini hakuwa akiwakumbuka hivyo alimwambia alimjibu hawakumbuki  kama hawakumbuki itakuwa ngumu kuwashitaki askari hao.

Wakili Kibatala alimuuliza shahidi huyo ana uhakika gani kama hao askari Polisi, ambapo alimjibu kuwa walitoka ndani ya Kituo cha Polisi Oysterbay na walikuwa wamevalia sare 'Uniform'.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alimuuliza shahidi huyo kwamba ni sahihi alipowaona Askari alikimbia na kukamatwa na alipelekwa Oysterbay Polisi, alijibu ni sahihi  na alidai kuwa ni kweli alipokuwa  Kituo cha Polisi alisikia mazungumzo ya waliokamatwa hlambapo walisikika wakisema kushangazwa na jinsi walivyokamatwa pamoja na mazungumzo ya Askari waliokuwa wakisema Askari wa Depo wameua mtu.

Pia shahidi huyo aliulizwa Askari waliomchukulia Hela alikutana nao chooni? alijibu alikutana nao kwenye Muembe wakati akielekea chooni. Kesi hiyo bado inaendelea

Mbali ya Mbowe, washitakiwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini,  Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Dk.Vincent Mashinji.

Washitakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad