Sheikh Kipozeo Ampa Neno Stamina..."Mwanamke Akikusumbua Mtafutie Mwenzake"



Hilal Shaweji maarufu kama Sheikh Kipozeo, amemshauri msanii wa HipHop Stamina juu ya kukimbiwa na mkewe na kumsihi atafute mwanamke mwingine kama amevunjiwa heshima ndani ya ndoa yake

Sheikh Kipozeo ameeleza hayo wakati akipiga stori na show ya Planet Bongo ambapo amesema wanawake wapo wengi na mungu amewaleta wawe wengi kuliko wanaume.

"Mimi namuhusia tu kwamba wanawake wapo wengi, kwahiyo ukiona mwanamke anakuvunjia heshima unatafuta mwingine tu, japokuwa yule aliyepita si kama wa huyu atakayempata sasa hivi, lakini utamzoea tu na atakuwa kama yule, sio jambo la kusikitika sana ndiyo maana Mungu amewaleta wanawake wengi duniani kuliko wanaume" amesema Sheikh Kipozeo.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad