MAGOLI manne yaliyofungwa na wachezaji wa Timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam Jonas Mkude , Medie Kagere ,Cloutus Chota Chama na Hassan Dilinga yametosha kuifanya timu hiyo kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba leo Januari 19, 2020 imejitupa kwa mara nyingine katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kucheza na timu ya Alliance FC ya Mwanza ambapo mchezo huo umefanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Katika. mchezo huo ulioanza saa 10 jioni timu ya Alliance ilikuwa ya kwanza kupata bao lake la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Patrick katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza .
Wachezaji wa Allince ambao walikuwa wanacheza kwa umakini mkubwa na kufanya mashambulizi ya kushitukiza kiasi cha kufanikisha bao hilo pekee kwa upande wao.Hata hivyo Simba aliamua kuangalia mbinu mpya ya mchezo ili kuhakikisha wanapata magoli.
Katika dakika ya 45 (+3) Simba kupitia mchezaji wake Jonas Mkude ilipata bao lake la kwanza na kwenda mapumziko kuwa ngoja droo ya 1-1.Kasi ya Simba iliyoambatana na kandanda safi lenye ufundi wa uhali ya juu ulioambatana na ari ya kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu walioongeza bao la pili kupitia kwa mshambiliaji wao hatari Mk 14 Medie Kagere katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili.
Wachezaji wa Simba hawakuishia hapo waliendelea kulisikama lango la Alliance na kupata bao la tatu dakika ya 64 kupitia kwa Mwamba wa Lusaka Chama na na dakika ya 73 walipata goli la nne kupitia kwa Hassan Dilunga. hadi dakika 90 zinamalizika za mchezo huo Simba 4 Alliance 1.
Pamoja na Simba kupata mabao manne katika i dakika 73,bado waliendelea kuonesha kiu ya kuendelea kutafuta mabao zaidi lakini walinzi wa Alliance walionekana kuuimarisha ulinzi.
Matokeo hayo ya Simba yaliyopatikana katika mchezo huo wa leo umeifanya kuwa na alama 41 kutokana na kucheza Michezo 16 hivyo kuendelea kujikita katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kabla ya mchezo dhidi ya Allince , timu ya Simba katika mchezo wake uliopita waliibuka na ushindi dhidi ya timu ngumu ya mbao Fc baada ya kuifunga mabao 2-1.
Hata hivyo Simba baada ya kumalizika kwa michezo hiyo ,sasa inarudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michezo mingine iliyopo mbele yake na hususani ule wa Kombe la Azam dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga.
Wakati Simba ikiibuka na ushindi kwenye michezo yake miwili iliyocheza jijini Mwanza ,watani wao wa jadi Yanga wamepoteza michezo yao miwili ikiwemo mchezo uliochezwa wiki iliopita dhidi ya Kagera Suger ambapo walifungwa mabao 3- 0 na jana imepoteza tena kwa kufungwa bao 1-0 na timu ya Azam FC.