Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo kwa raia wake kuingia Marekani, Sababu zaelezwa


Kwa taarifa ambazo zinazidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi leo ni kwamba, Serikali ya Marekani ina mpango wa kuziongeza Nchi nyingine 7 ikiwemo Tanzania kwenye orodha ya Nchi ambazo Raia wake wanatarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Nchini humo.

 

Katika taarifa hiyo inaeleza kuwa nchi nyingine 7 ambazo zinztarajiwa kuwekewa vikwazo ni pamoja na Nigeria, Sudan, Eritrea, Myanmar, Belarus na Kyrgyzstan.

Kwa mujibu wa Vyombo vya habari vya nchini Marekani vimeripoti kwamba baadhi ya Nchi VISA zinaweza zisifungiwe kabisa bali zitakua ngumu kupatikana kwa masharti zikiwemo VISA za biashara na za matembezi.

Idara ya mambo ya ndani ilipotafutwa na Waandishi haikuwa tayari kujibu chochote kuhusu hili lakini kwa upande mwingine Maafisa kwenye Uongozi wa Rais Trump wamesema bado orodha haijakamilika kwani mpaka Jumanne jioni Ikulu ilikua bado inajadili kuongeza ama la Nchi nyingine moja au mbili ambapo pia Nchi nyingine kwenye hii orodha zitafungiwa kushiriki bahati nasibu ya Green Card.

Ripoti imesema baadhi ya Nchi hizi 7 Raia wake wameongoza kwa kupitiliza muda wa kukaa Marekani kulingana na VISA walizopewa ambapo kwa mwaka 2018 asilimia 24 ya Raia wa Eritrea walipitiliza siku za kukaa Marekani, Nigeria 15%, Sudan 12%.

Chanzo: (THE WALL STREET JOURNAL) 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad