Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema ufungiaji wa laini ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanywa kwa awamu kuanzia jana kwakuwa wakifungia laini zote kwa wakati mmoja wataongeza mzigo kwa wanaosajili na mfumo wa usajili utaelemewa “hadi jana saa nne usiku tulikuwa tumezima laini 975,041” .
“Kundi la kwanza tulilowazimia laini ni Watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya Taifa au namba lakini hawajasajili laini zao, kundi la pili ni Watu 318,950 waliosajili laini zao kwa vitambulisho vya Taifa kabla ya kuanza kwa mfumo wa kusajili laini kwa alama za vidole”- TCRA