TMA yatangaza tukio la Kupatwa kwa Mwezi



MAMLAKA ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza tukio la kupatwa kwa mwezi kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 2:07 usiku wa Januari 10 hadi saa 6:17 usiku wa kuamkia Januari 11, 2020.

Taarifa hiyo ya kupatwa kwa mwezi imetolewa leo Januari 9, 2020 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Utabiri wa Kituo Kikuu cha Utabiri, Samuel Mbuya ambaye ameongeza kuwa, tukio hilo ni la nadra kutokea kwa muda mrefu hivyo amewataka watanzania kushudia sayansi hiyo ya anga.

Amesema, tukio hilo litaonekana katika sehemu kubwa kwenye nchi ambazo muda huo utakuwa usiku hasa Ulaya, Asia, Australia na Afrika..embako  tukio huonekana wakati dunia, mwezi na jua vikikutana kwenye mstari mmoja mnyoofu na Kutokana na hali hiyo kupatwa kwa  mwezi kwa maeneo yaliyo mengi huonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mng’aro wa mwezi.

"Mwezi huanza kupungua mng'ao wake na kuwa giza kabisa kwenye uso wa dunia kwa muda kisha hurudi kwenye hali yake ya kawaida, hakuna athari kubwa zinazoweza kutokea ingawa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji baharini kwa sababu ya mvutano kati ya maji na mwezi kwenye bahari," alisema Mbuya.

Aidha mtabiri hugo amewashauri wanafunzi wa masomo ya sayansi kufuatilia tukio hilo la kidunia na kujifunza zaidi kuhusu sayansi ya anga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad