Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro ameiambia JamiiForums kuwa kila mwaka Wazazi hufanya sherehe kubwa kwa ajili ya Watoto wao waliomaliza Elimu ya Msingi
Amesema, sherehe hizo si kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuhitimu Elimu ya Msingi bali kwa lengo la kuwaingiza kwenye ndoa Watoto wa Kike na wa Kiume kuwatumia katika kazi
Wilayani humo, kila mwaka siku ya mtihani wa mwisho wa kumaliza Darasa la 7 wazazi huzingira shule za Msingi wakiwasubiri Watoto wao kwa ajili ya kuwalaki
Wazazi hushona sare na kuandaa sherehe kubwa, watoto wakitoka kwenye mtihani hupokelewa kwa shangwe na maandamano ya kuelekea nyumbani hufanyika
Watoto hao wakichaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza, Wazazi hudai hawana fedha. Mkuu wa Wilaya hiyo Julius Mtatiro amesema mwaka huu hakutakuwa na sherehe hizo
Aidha, Mtatiro ameeleza kuwa Wanafunzi wote waliomaliza Darasa la Saba Wilayani humo, wamefaulu na kukidhi sifa za kujiunga na Kitado cha Kwanza na atahikikisha wanajiunga na shule