'Ubwege Unalinda Mapenzi, Mke Wangu Nampikia na Kumfulia' - AT Afunguka


Msanii wa muziki nchini AT, amesema kuwa yeye amemzuia mke wake kuingia jikoni kupika, badala yake yeye huwa anampikia na hata kumtandikia kitanda, kwa kuwa wanawake duniani hawajaletwa kuteseka bali kupendwa na kuhudumiwa.

AT ameyabainisha hayo katika kipindi cha DADAZ, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kupitia East Africa Television, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 6:00 mchana.

"Mke wangu ana roho ya kipekee sana, alishawahi kuwekewa sumu na akasamehe, mke wangu kwanza hapiki nilimzuia, mimi ndiyo nampikia,namfulia na kumtandikia kitanda, ubwege siku zote unalinda mahusiano"amesema AT.

Aidha AT amesema kuwa wanawake wengi huteseka kwenye mahusiano kwasababu wao wametokana na binadamu, ndiyo maana wana huruma,ukilinganisha na wanaume ambao wametokana na udongo ambao kwa asilimia kubwa hawana huruma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad