Uingereza Yashtushwa na Tangazo la Iran


Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kuwa tangazo la Iran la kuacha kuheshimu kikomo cha urutubishaji wa urani ni jambo linalotia wasiwasi.

Msemaji huyo ameongeza kuwa Uingereza kwa sasa inafanya majadiliano na wahusika juu ya hatua zinazoweza kuchukuliwa.

Amesema pia kwamba nia ya kila mmoja ni kuhakikisha kwamba mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 unaendelea kuwepo.

Msemaji huyo hali kadhalika amezungumzia kitisho ch Rais wa Marekani Donald Trump cha kuzishambulia turathi za utamaduni wa taifa la Iran, akisema yapo makubaliano ya kimataifa ya kuzuia uharibifu wa turathi za namna hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad