UKWELI Mchungu...Kuna Watu Wamefungwa na Familia zao Wasioe Ama Kuolewa


Hili jambo ni mpaka likukute ndiyo utaona madhila yake, la sivyo utaona ni story tu.

Kuna baadhi ya familia hutokea mtoto mmoja akainuliwa kuliko wengine, na yeye kwa kupenda ama kinyume chake, asifanye juhudi zozote kuwainua nduguze.

Huyu mzazi humuona kama ndio mkombozi na kichumio cha familia.

Wote tunatambua dhima, hamu na furaha ya kuwasaidia ndugu na wazazi mara upatapo kazi, biashara kustawi n.k na ukiwa bado single. Wengi huwaza nyumbani kwanza, wazazi na ndugu.
Hapa ni kwa vile bado huna kwako rasmi.

Wazazi wengi hulitambua hili na wachache hupenda kudiriki kusema: "Akipata kwake huyo hatatujali tena kama zamani", ama watasema "ameshapata kwake huyo huduma zimepungua na hatujali tena" Hii hofu wanayo wazazi wengi.

Ni ukweli usiopingika na jambo lisilozuilika tena unapompata wako wa kujenga kwenu nyie wawili sasa. Mambo hubadilika kwa kasi sana. Ukiamka badala ya kuwaza wazazi sasa, ama ndugu zako, cha kwanza utamuwaza mwandani wako. Ni wachache mno mno huweza kubalance hili.

Taratibu ukaribu huanza kupungua kati yako na familia yako ya wazazi na ndugu na ombwe kuanza kuonekana. Na kama ni familia iliyobweteka na haijitumi halafu wewe ndiyo kila kitu kwao, tatizo huwa kubwa maradufu.

Sasa basi baadhi ya wazazi, sometimes kwa msaada wa ndugu kwa kuogopa kukosa ukaribu walio uzoea, huamua kutumia nguvu za giza kukufunga ili usiweze kuoa wala kuolewa. Sana sana utaishia tu ku-date na watu kwa muda mfupi na mwishowe mahusiano kufa bila sababu zozote za msingi.

Unaweza kujikuta kabisa unatamani kuwa na familia yako baada ya kumpata mtu sahihi lakini the moment unawashirikisha wazazi na ndugu zako, matatizo huanzia hapo. Mwishowe wanaku-counsel kuwa huyo siyo mtu sahihi kwako nk nk. Unajikuta unampiga chini na mambo yako yanarudi kwenye mstari. Hapo lazima uwaamini ndugu zako.

Mzazi ni Mungu wako wa pili, usipomsikiliza yeye au akikunenea mabaya unaweza usifanikiwe maisha yako yote! Lakini je kama ukigundua ni kimeo? Je, utafanyaje ukigundua kuwa mzazi hataki uwe na mahusiano rasmi?

Ndiyo maana kuna baadhi huamua kwenda mbali na nyumbani na kufanya baadhi ya vitu kimyakimya bila kuwashirikisha wazazi na ndugu. Akishajiweka vizuri kabisa ndio hurejea akiwa tayari na kwake kulikosimama!!
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad