Ushauri: Mume Hataki Kufanya Mapenzi na Mimi, Anamtaka Mtoto Niliyezaa Kabla ya Kunioa

Naombeni ushauri wenu,

Mawazo ya wengi ndio nitakayoyafanyia kazi. Nimefunga ndoa na mwanaume mwenye watoto 4 wawili wakike wawali wa kiume. Mama yao alifariki kwa ajali ya gari aliwaacha wadogo wakiwa primary.

Na mimi niliolewa nikiwa na mtoto mmoja wa kike ambae kiumri analongana na mtoto wake watatu. Kusema ukweli mwanzoni iliniwia ngumu sana kukubali ombi lake hasa nikifikiria kulea watoto wa mama mwingine wanikubali, je, vipi kuhusu huyu nilienae?

Baada ya muda kupita na kukolea kimapenzi nilijubaliana nae tukafunga ndoa tukaunganisha familia wote wakawa kitu kimoja. Mungu akabariki tujaliwa kupata mtoto mmoja. Kiukweli niliwapenda sana hawa watoto, niliwalea kama wangu.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwafanya wasijione wakiwa. Kama zawadi nk nilitowa mezani bila kubagua sikupenda kuweka makundi na hili shahidi ni Mungu pekee. Watoto watatu wapo chuo kikuu na mmoja wa kwake yupo form six.

Katika ndoa yangu kulikua na migongano upande wa tendo la ndoa, kabla ya ndoa tukiwa kwenye stori za mapenzi niliwahi kumweleza mwenzangu kuwa mimi sio mtundu sana upande wa sex ivyo ningependa yeye awe mwalimu kwangu kwani tangu mwanaume wa kwanza anidanganye na kunipa ujauzito sikuwa tena kuwa na byfriend.

Akiniambia sawa. Tulipoingia kwenye ndoa mwenzangu alianza kubadilika wakati mwingine alikaa hata miez 8-10 bila kutaka sex.Nikimuuliza husema amechoka au hajisikii.

Hata huo muda anaokaa mpaka mimi nimchokoze na hii nikutakana na kushindwa kuvumilia. Kuna wakat aliamua kuniambia ukweli kuwa sijui mapenzi, niliumia ila nilikubali kuwa ni kweli sijui ila anisaidie kujua.

Hakufanya ivo. Ilifikiwa wakati nikaona ngoja nikae nisimsumbue ila nilijiuliza nitaishi hivi mpaka lini na kusaliti ndoa siwezi. Nilimwomba Mungu sana anipe uvumilivu ila pia Mungu aseme na mimi juu ya hii ndoa.

Mungu ni mwaminifu. Baada baada ya maombi ya zaidi ya mwaka mke wa shemeji yangu alileta malalamiko kuwa mume wangu amekua akimsubua sana kimapenzi ikiwa ni pamoja nakumtumia picha za ex.

Niliziona hakuishia hapo akasema hata hawa wadada wa kazi huwa anatembea nao. Nilipowabana waliopo na walioondoka walikubali na kunipa ushahidi. Mbaya zaidi hata huyu mwanangu alishamtaka kimapenzi sina uhakika kama alifanikiwa au la.

Ninaumia sana sana. Mtaani ndoa yangu imekua mfano wa kuigwa hio ni kutokana na jinsi tunavoonekana kwa watu. Lakini hii yote onatokana na jinsi nisivopenda watu wajue mambo ya ndani. Ninampenda, ninamheshim, ninamjali.Siruhusu nguo au chakula cha mume wangu afanye mwingine nikiwepo.

Hata kama tumegombana nisingependa yoyote ajue, nilijitahidi sana, kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwake. Hii nikutokana na malezi niliyolelewa. Hata kama amesafiri watoto watajua baba anarudi kwakua wataniona jinsi ninavokua busy jikoni na kuandaa juisi na matunda.

Ushauri wenu muhimu sana kwangu

Asanteni
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KKKKKKKKKKKKKKKKKKK

    ReplyDelete
  2. huyo hakupendi

    ReplyDelete
  3. Achana nae, asije kukuletea virusi bure. Amekuvunjia heshima vya kutosha

    ReplyDelete
  4. Pole sana dada ila inavyoonekana siyo kwamba hujui mapezi .Ila jamaa anakatabia Fulani ambako mke wake wakwanza huenda alikuwa anavumilia au alikuwa hajui.Sasa kumbuka tayari umeshazaa naye watoto wawili hiyo tayari imeshakuwa familia.Unachotakiwa wewe endelea kuwa mvumilivu wala usije ukaiga tabia yake kwa kulipiza, pia take time tafuta wazee wa mbali sana waje wamshauri ili nawe uweze kufurhia ndoa yako.

    ReplyDelete
  5. Dada kwa ushauri zaidi simama katika neno hilo ndiyo kimbilio lako.Maana hizo ni nguvu za shetani .
    For more counseling 0757325596

    ReplyDelete
  6. Pole sana mama! Mungu uliyemuomba sana na akakufunulia siri hiyo, ni Mungu huyohuyo umkabidhi tatizo hilo la Mumeo. Naamini kabisa kwa maelezo yako ya jinsi unavyompenda na kukaa katika Imani thabiti ya kumsitiri mumeo Mungu atageuza ubatili wote wa mumeo na kumleta kwako. Usihangaike kuwa hujui mapenzi, kwani mapenzi hayana mjuzi, hiyo ni Sanaa ambayo kila kitu kinapatikana uwanjani kutegemea wachezaji wenyewe. Mungu hatakuacha kamwe endelea kumuombea sana.Usijemkimbia kwani waweza kuruka tope ukaenda kukanyaga mavi. Muhimu sna ni kulinda afya yako yaani hakikisha kondomu imevaliwa siku akikutokea kukuhitaji kimwili. Nitajiunga nawe katika kukuombea kwa jambo hili.Ubarikiwe sana!

    ReplyDelete
  7. pole sana dada hayo ni majaribu na ni mtihani kwetu c wanandoa usije sema unalipiza kisasa muombe sana Mungu wako. atakusidia

    ReplyDelete
  8. Pole sana,huyo mme wako ana pepo la uzinzi,mpeleke akaombewe kanisani

    ReplyDelete
  9. Huyo mume anaonesha mhuni ikiwa ni kweli anamtaka hata mwanae na Hana shukura kwa yote unayomtendea yeye na watoto wake. Utavumilia huyo kuwa mumeo na wakati uleule kufanya mapenzi na mwanao uliemzaa. Huyo si mume na subira pia ina mpaka lakini siwezi kukushauru kutokana nae lakiniiipo dini tukufu ambayo. inasema pindi ikifika miezi mitatu akashindwa kumpa mkewe haki yake Bila ya sababu kinaisha basi mke huyo kaachika

    ReplyDelete
  10. Binafsi nyote nawaona misukule tu maana mwanadam wa kawaida hawezi kuishi bila tendo la ndoa kwa miez8

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad