Usipime Harmonize Kupiga Show 02 Arena 2020 Uingereza



KWENYE tano bora ya wasanii wanaopeperusha bendera ya Tanzania kwenye Muziki wa bongofleva huwezi kumuacha kumtaja msanii Rajab Harmonize.

Harmonize alipokua akifanya mahojiano na kituo cha redio nchini amesema kwa mwaka huu anatarajia kufanya show yake katika ukumbi wa 02 arena uliopo nchini uingereza huku akiweka wazi kuwa malipo tayari yameshafanyika yeye kufanya show hiyo juni mwaka huu.

"Natumaini nitaweka historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki kufanya show katika ukumbi huo mkubwa wa burudani,"

Aidha, harmonize amefafanua kuwa alipokua uwanja wa vila pack kwenye mechi ya leister city dhidi ya Aston Villa alishuhudia shangwe na vifijo pale mchezaji kutoka nchini Tanzania Mbwana Samata alipoingia uwanjani kwa mara ya kwanza mara baada ya kusajiliwa na klabu ya aston Villa.

"Juzi nilivokua uwanjani nilithibitisha hilo kwani ndio mara yake ya kwanza kuingia dimbani kupitia timu ya Aston Villa tangu asajiliwe lakini bado mashabiki walikua wakipiga yowe na wakitaja jina lake wakiwa na imani nae jambo kama hilo linatia sana hamasa sana kwake na kitaifa pia kuona hatuangushi hasa kwenye sekta ya michezo na kuipeperusha bendera ya Tanzania,"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad