MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania(TCRA) inaendelea kuwakumbusha wananchi kuwa zimebakia siku tatu lakini naona kama watu kama wengi bado huku tukiona misululu katika mamlaka za vitambulisho vya taifa NIDA.
Sina hakika kama kweli NIDA wataweza kuhudumia watu wanaoongezeka kila uchwao kwa huku mjini tuu.
Huko vijijini pia sidhani kama wote wanaweza wakawa wamepata hata hizo namba za utambulisho wa taifa kwaajili ya kusajili laini za simu.
Sipati picha kwa wale wananchi wa kijiji cha Mfyome kilichopo tarafa ya Isimani jimbo la Kalenga kata ya kiwele wilaya Iringa vijijini wanapopanda vidarara vidogo vya buku jero kwenda NIDA kutafuta japo namba tuu wasajili laini.
Laini ambazo zitaweza kuwasaidia kuwasiliana na watu mbalimbali wakiachana na kurudi na zama za Kutuma barua kwa kutumia P.O.BOX zao ambazo zinaweza zikawa zimesahaurika kutokana na urahisi wa mawasiliano kwa mtu mmoja mmoja.
Licha ya kuwa baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mfyome washasajili laini zao na kuwasaidia wengine kuwasajilia kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine.
Sijajua vizuri kama kumsajilia mtu laini ya simu ni halali au si halali lakini kinachopaswa ni kila mtu awe na kitambulisho cha taifa kutoka mamlaka ya vitambulisho NIDA.
Hata hivyo tumshukuru Rais wa wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza siku la sivyo kuna wananchi ambao wangekuwa washaanza kutuma barua zao ili kumfikia jirani yake ili ujumbe umfikie mhusika.
Tofauti na hapo awali walipokuwa wanaweza kuwasiliana kwa kupigiana simu au meseji ya kawaida ili kufikisha ujumbe kwa mhusika.
Ukizingatia ili kupata kitambulisho cha Taifa kila mmoja lazima atoe taarifa sahihi kuhusu yeye sijui wale mzee wa kijijini kama amefanikiwa kupanda daradara ya buku jero kufika NIDA kutoa taarifa zake ili kupata japo namba za kitambulisho ili waweze kusajili laini yake.
Achana wale wazee vipi kwa vijana wanao timiza miaka 18 baada ya tar 20 kufungwa kwa laini, hima waende NIDA ili waweze kupata namba zao ili waweze kwenda kuaajili laini waweze kuwa na mawasiliano kama wanahitaji.
Kwa upande wangu nafikili kila mtu akisajili laini yake na kuweza kutumia huduma za simu anaweza kuweka vocha na kutumia huduma ya miamala ya pesa basi TRA itanona mapato kwani kila vocha kiasi fulani kinakatwa kama VAT basi nchi yetu itaendelea kupendeza kwa kuwa na barabara Nyeusi kila kona kama ilivyo kijichi.
Hili ni wazi kabisa kuwa wasio sajili laini zao kwa alama za vidole tutakuatana zama za barua za kirafiki vile tutakuwa tukitumiana barua kw njia ya kuagiza kwa mtu au kutuma kwa kutumia P.O.BOX kama nilivyoandika hapo awali, ingawa zimebaki siku tatu za kufungwa kwa laini kwa wasiosajili kwa alama za vidole.