Vita ya Viungo Simba vs Yanga...Niyonzima Kaleta Balaa



Katika mchezo wa Jumamosi iliyopita  wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga, kulikuwa na vita kubwa ya katikati ya uwanja. Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.

 

Tazama hapa jinsi ilivyokuwa: SIMBA Clatous Chama Jumla ya pasi ni 40, kuharibu mipango mara moja, hajapiga pasi ndefu. Shuti lililolenga lango ni moja. Jonas Mkude Jumla ya pasi 56, kuharibu mipango mara tatu, pasi ndefu tatu, kupoteza moja.

 

Mzamiru Yassin Jumla ya pasi 49, kuharibu mipango mara moja, pasi ndefu tatu , kupoteza moja. YANGA Balama Mapinduzi Alimaliza mchezo huo akipiga jumla ya pasi 36.

 

Mashuti alipiga matatu, moja likalenga lango na kuwa bao. Abdulaziz Makame Alipiga jumla ya pasi 21, akaharibu mipango ya timu pinzani mara tano, akapoteza pasi saba, akafanikiwa kupiga pasi za mbali mbili. Haruna Niyonzima Jumla ya pasi ni 53, amepoteza tatu, pasi ndefu mbili, kuharibu mipango mara tatu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad