Wakili Jebra Kambole Afunguka "Tayari Tumempa Taarifa za Msiba Erick Kabendera Gerezani"



Wakili Jebra Kambole  amesema tayari wamempa taarifa ya msiba wa Mama yake Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera ambae yupo Gerezani.

Wakili Kambole ambae anamtetea Kabendera kwenye kesi ya utakatishaji fedha iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amesema wanafanya utaratibu kuona kama atashiriki maziko "kuna Logistic za kufanya ili Kabendera aweze kushiriki msiba ila tunazungumza na Ndugu tuone wanasemaje"

"Kabendera amezipokea kwa masikitiko sana taarifa hizi sababu Marehemu ni Mtu ambaye alikuwa anamtegemea, amewashukuru Watanzania kwa mchango na pole wanazompatia" - Wakili Jebra Kambole
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad