Walimu, Wanafunzi Wamiminika kwa Mwanafunzi Aliyepata One ya 7



WALIMU na wanafunzi wa Shule ya Sekondari- Igaganulwa (shule ya kata) iliyopo Bariadi vijijini -Mkoani Simiyu wampongeza Kijana Yohana Lameck Lugedenga ambaye amefaulu kwa kupata alama A kwenye masomo 9 na kuibuka na ‘division one’ ya point 7.

 

Pongezi hizo zilitolewa jana  Januari 14, 2020 na Waalimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kijana wa miaka 19 Yohana Lameck Lubelega ambaye ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto wanne.



Yohana amesema, kusoma kwa bidii, kuwa na ratiba na kuhakikisha kuwa unaifuata ndio siri kubwa ya mafanikio. Alielezea kuwa ndoto yake ni kuwa daktari ili kuwasaidia wanainchi wenye matatizo ya afya.

 

Akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne 2020 aliwasisitiza kuwa na nidhamu, kuwa na ratiba ya kujisomea na kuizingatia.

 

Akizungumza mwalimu wa somo la Kiswahili Mwl. Baraka Godfrey alieleza; “Yohana amenibeba kwani kwa kipindi kirefu sana hakujawa na alama A katika somo la kiswahili. Shukrani za dhati zimuendee Rais, John Pombe Magufuli kwa kuruhusu elimu bure kwani bila hivyo ingekuwa vigumu kwa watoto kama Yohana kupata fursa hii.


“Shukrani zimuendee Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka kwa kuanzisha makambi ya wanafunzi kwani yamechangia kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi. Yohana in kijana mtiifu sana na nimekuwa karibu nae sana,” alisema Mwalimu Baraka.

 

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Igaganulwa, Mwl. Emelius Emmanuel John alieleza: “Ufaulu wa Yohana umedhihirisha kuwa hata shule za Serikali/za kata tunaweza, pamoja na changamoto mbalimbali endapo waalimu na wanafunzi watajitahidi kila mmoja kwa sehemu yake basi kwa hakika tunaweza na tutaweza.


“Shule ya Igaganulwa ina changamoto ya waalimu,kwani tuna waalimu 12 tu na mmoja yupo masomoni. Mwaka 2019 wanafunzi 88 walifanya mthihani kidato cha nne,ambapo Mwanafunzi mmoja alipata daraja la kwanza kwa point 7 ambaye ni Yohana,” alisema Mkuu wa Shule.

 

Wakizungumza Mama ya Yohana-Bi. Masalu Lyalya na bibi mzaa mama Bi.Mbhuke Limbu, walimtaka Yohana a some kwa bidii ili hatimae aisaidie familia yake.

Ili kumsaidia Yohana, Namba ya Akaunti ya benki ni 30510022929

Benki ya NMB

 

MAMA MZAZI WA YOHANA LAMECK AMFUNGUKIA RAIS MAGUFULI!


Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera sana kijana kwa ufaulu wa hali ya juu.

    ReplyDelete
  2. Hongera Sana kijana, piga shule Kwa nguvu na moyo wako wote na mafanikio yako utayaona baadaye.

    Nakutakia kila la kheri unapoanza Safari yako hii ya elimu.

    ReplyDelete
  3. Vyema sana mtoto mzuri. Mtangulize mungu katika masom yak

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad