Waliosajili Kwa Vitambulisho sio vyao Kuondolewa



Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA),kwa kushirikiana na watoa huduma itafanya zoezi la kuhakiki laini zote na kuwaondoa wale waliosajili laini zao kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine au kitambulisho tofauti, pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba, imeeleza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kujiridhisha kama waliosajili laini zao za simu wametumia vitambulisho sahihi.

Na kwamba TCRA wataendelea kutoa onyo kali kwa wale watakaotumia vitambulisho visivyowahusu wakati wa usajili wa laini zao.

Aidha kwa wale waliositishiwa huduma za laini zao, wanaweza kuendelea na utaratibu wa usajili kwa lengo la kurudisha laini zao zilizofungwa au kupata laini mpya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad