Wanafunzi wa Sekondari Waharibu Madarasa kwa Kuandika Matusi Wazazi Kugharamia Ukarabati


Familia mbili za watoto wanaosoma shule ya sekondari Nyihogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga zimetakiwa kugharamia uharibifu wa miundombinu ya madarasa ya shule ya msingi Nyihogo baada ya watoto wao kuiharibu kwa kuandika matusi ya kuwatukana walimu wa shule hiyo ya msingi.

Akizungumzia hatua hiyo mwenyekiti wa mtaa wa Bukondamoyo Frank Mabugi amesema baada ya uharibifu huo kufanywa serikali ya mtaa imewataka wazazi wa watoto kugharamia sehemu iyoharibiwa kwa kila familia kulipa kiasi cha shilingi 80,000 na ilipwe Februari 5, 2020.

Mabugi amesema sehemu iliyoharibiwa ni ukuta wa vyumba viwili vya madarasa ambayo bado mapya toka yamekamilika kujengwa na watoto waliofanya tukio hilo wanasadikika wamesoma katika shule hiyo ya msingi Nyihogo ili kufidia uharibifu huo jumla ya fedha ni shilingi 160,000 inahitajika ambapo wazazi wa watoto hao watailipa.

Amesema wakati tukio hilo linafanywa na wanafunzi kuandika matusi kuna baadhi ya watoto 23 ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Nyihogo waliwaona huku wakipewa vitisho ili wasitoe taarifa lakini licha ya kupewa vitisho hivyo walisema na uongozi wa mtaa kuwabaini wazazi wao.

“Tumekutana na wazazi wa watoto hao waliotuharibia miundombinu yetu na tumefikia muafaka kwanza tumeangalia uharibifu wote na kuangalia gharama ya vifaa pamoja na malipo ya fundi na kiasi cha shilingi laki moja na sitini elfu hivyo wameahidi kuilipa ili kufidia”.

Kwa upande wao wazazi wa watoto hao wamesema kiukweli tabia hiyo sio nzuri na baada ya taarifa hizo ziliwashtushwa hivyo kwa ujumla wanakiri kulipia gharama zote na watahakikisha tabia hiyo haijirudii huku wakiwataka wazazi wenzao kuwa waangalifu kwa watoto.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad