Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema Serikali itaanzisha mfumo wa bima kwa wananchi mkoani humo ili wawe na uhakika na upatikanaji wa huduma za afya kwa kuchangia kiasi kidogo cha pesa.
Mrisho Gambo ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Arusha, ambayo inasubiliwa na wananchi kwa muda mrefu.
"Uboreshaji wa miundombinu ya Afya, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Arusha, utapunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wananchi na baada ya hapo tutawahamisha wananchi waanze kutumia bima" amesema RC Gambo.