Wanusurika Baada ya Kupigwa Risasi na Polisi Geita



WATU wanne wakazi wa Kitongoji cha Kamlale Kijiji cha Kibwela Kata ya Nyawilimilwa, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, wamelazwa katika Hospitali Teule ya Rufaa Mkoa wa Geita  wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya kupigwa risasi za kifuani na mikononi na baadhi ya polisi wa Kituo kidogo cha Nyawilimilwa.

 

Tukio hilo limetokea jana muda mfupi baada ya watu zaidi ya 200, kufika katika kituo hicho cha polisi kwa lengo la kutaka kujua sababu za jeshi hilo kumkamata Mwenyekiti wao wa Kitongoji cha Kamlale Alex Abel, ambaye alikamatwa majira ya alfajiri akiwa nyumbani kwake kijijini hapo.

 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, amekiri jeshi hilo kuwajeruhi kwa risasi wananchi hao kwa madai kuwa wasingeweza kuwavumilia watu ambao lengo lao lilikuwa kuvunja kituo na kuharibu mali zilizomo.

Aidha polisi waliwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na majeruhi hao waliolazwa hospitalini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad