Maafisa wa polisi nchini Kenya, wamewakamata watu watano waliokuwa wanashukiwa kutekeleza shambulizi la kigaidi jijini Nairobi, baada ya kupata taarifa muhimu za kijasusi.
Ripoti za polisi zinasema kuwa, washukiwa hao ni wanaume watatu, na wanawake wawili raia wa Marekani, Somalia na Kenya.
Polisi wanaamini kuwa washukiwa hao walikuwa wanapanga kwenda kutekeleza shambulizi hilo Kaskazini mwa jiji la Nairobi wakilenga kilabu moja ya pombe katika barabara ya Kiambu.
Maafisa wan usalama wameimarisha usalama katika jiji hilo kuu, baada ya washukiwa wa Al Shabab kutoka Somalia hivi karibuni kutekekeleza mashambulizi katika kaunti ya Lamu pwani ya nchi hiyo na Garissa Kaskazini Mashariki karibu na nchi ya Somalia.
Al Shabab imetishia kulengamalshi ya kenya na Marekani, kutokana na mataifa hayo mawili kuendelea kuwa na wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wake.