Wastara Amlilia Tena Sajuki ‘Alikuwa Mguu Wangu’



MSANII wa Bongo Movies na mjasiriamali, Wastara Juma ameamua kufunguka tena wakati akikumbuka kifo cha mumewe, Juma Issa Kilowoko (Sajuki) na kuwaomba watu na ndugu waendelee kumuombea kipenzi chake huyo.

 

Wastara kupitia akaunti yake ya Instagram amesema Sajuki alikuwa kila kitu kwake, na hata alipokatwa mguu baada ya ajali, mwanadada huyo hakuona shida kwani mumewe (Sajuki) alikuwa ni kama mguu wa pili na kufanya Wastara awe na faraja na furaha muda wote.

 

LEO 2/1/2020 NI KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MAREHEMU JUMA JUMA ISSA KILOWOKO (SAJUKI) AMEFIKISHA MIAKA 7 TOKEA ATUACHE SOTE TUMUOMBEE INSHAALLAH

Nakumbuka siku ya tal 1/1/2013, Sajuki alikuwa amelazwa Muhimbili Hosptal, aliniambia ‘unajua mke leo nimeuona mwaka mpya hata nikifa muda huu nitasema na mimi nilikufa mwaka mpya’.

 

Halafu akasema ‘Mke wangu unajua imebadilika number tu lakini maisha ni yaleyale, kilakitu kiko vilevile na mimi niko hapa hapa kitandani sina hata mabadiliko, walau ningeweza kuinuka tu nikakupeleka out ningesema mwaka umekuwa mpya na mambo mapya’.

 

Hii kitu imeniharibu sana, sionagi kwangu kama mwaka mpya ni kitu kipya ila naona ni kitu chenye kumbukumbu mbaya sana kwangu, watu wanaumiaga kufiwa na wazazi na mume lakini mimi kwangu huyu jamaa alikuwa mguu wangu wa pili uliokatika nikaona yeye ndio amesimama kwenye hiyo nafasi.



Nilijiona mzima na nina miguu yangu yote miwili na sijawahi kujiona kuwa nina mapungufu ya mguu mmoja mpka siku alipoondoka mume wangu kipenzi Sajuki ndiyo niliona mapungufu yangu yooote hata mengine nilijiongezea tu mwenyewe akilini mwangu.

 

Watoto wako wanakuombea sana, mimi sijaaacha kukuombea na sitaacha mpka siku nitakayokuja huko ulipo. Ulimuacha bint yako mdogo wa miezi 7, sasa hivi amekuwa na anajua ulikuwepo na umeondoka, anakuombea kila siku ili urudi, hajui kama wewe huwezi kurudi ila sisi ndio tutakuja ulipo.

 

Tunakupenda sajuki wetu, Mungu akulaze mahali pema peponi, amiin amiin sote tuseme amiin tuendelee kumuombea Sajuki.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad