Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Bw. Filberto Sanga amewataka Watendaji wa Kata, Vijiji na Wataalam wengine kujieupusha na tabia ya kuchukua fedha kwa wananchi ili wawapatie fomu za kitambulisho cha taifa NIDA.
Mhe. Sanga amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliolenga kusikiliza kero za wananchi wa eneo hilo, ambapo amesema yeyote atakayekutwa akifanya hivyo serikali haitosita kuchukua hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Amesisitiza kuwa tabia ya wasimamizi wa NIDA kwa ngazi ya kata na vijijji kuwauzia fomu wananchi haikubaliki kwani huduma hiyo hutolewa bure hivyo yeyote atakayebainika serikali haitosita kuchukua hatua kali.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wananchi wa Mwandege kujitokeza kushiriki katika zoezi la urasimishaji ardhi pindi zoezi hilo litakapoanza huku akiwataka wale wote watakaotakiwa kupisha ujenzi wa miradi ya maendeleo kuwa na moyo wa uzalendo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.