Watu wasiojulikana wameiba mashine zote za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Arusha


Watu wasiojulikana wameiba mashine zote za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) zilizokuwa katika Ofisi za NIDA za kituo kidogo cha Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo, kituo hicho kimefungwa kwa leo na Polisi wameanza mchakato wa kuwasaka waliohusika na wizi huo.
"Vifaa vyote vimeibiwa, kompyuta nne, camera si chini ya tatu na vifaa vingine vyote, tumepata mshtuko, milango haikuvunjwa inaonekana ni wizi wa kimkakati umefanywa ndani, vifaa vya NIDA ni  mali za Taifa sasa hawa wanapata wapi ujasiri wa kuiba!"- Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya Arumeru
  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad