Watuhumiwa 5 wa IS Wakamatwa Uturuki



Polisi kwenye mji mkuu wa Uturuki, Ankara wamewakamata watu watano wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS kwa madai ya kupanga mashambulizi katika mkesha wa Mwaka Mpya.

Shirika la habari la Uturuki, Anadolu limeripoti kuwa watuhumiwa hao ni raia wa kigeni wanaofungamana na makundi ya kigaidi nchini Syria na Iraq.

Anadolu imesema msako wa polisi unaendelea na kwamba huenda watu zaidi wakakamatwa.Taarifa hiyo imetolewa wakati hatua za kiusalama zikiendelea kuchukuliwa nchi nzima kabla ya sherehe za Mwaka Mpya.

 Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki, zaidi ya askari 317,000 wa usalama wametawanywa nchini humo.

Jana, shirika la Anadolu liliripoti kuwa zaidi ya watu 100 wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa IS wakiwemo takriban raia 50 wa kigeni, walikamatwa katika msako unaoendelea nchi nzima.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad