Watumishi sita wanaokusanya ushuru wa serikali katika halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa shilingi milioni mia moja kumi na tisa baada ya kuharibu mfumo wa ukusanyaji wa mapato kupita mfumo wa mashine maalumu zinazotumika kukusanya ushuru.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua Dk.John Pima amesema uamuzi wa kuwafikisha mahakamani umetokana na serikali kubaini upotevu wa kiasi hicho cha fedha uliofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo wasiokuwa waadilifu.
Akikabidhi mashine mpya arobaini na tatu za ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kaliua katibu tawala wa wilaya hiyo Michael Nyahinga amesisitiza halmashauri hiyo kubuni njia zaitakazosaidia kuziba mianya inayotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waadilifu kufanya udanganyifu.