Waziri Mkuu Atoa Agizo kwa Wazazi Wenye Watoto Wanaosoma China


Waziri Mkuu Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wazazi ambao wana watoto wanaosoma  China na sasa wapo nchini Tanzania wasiwarudishe watoto hao nchini huko mpaka pale hali itakapokuwa sawa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa ambao umekuwa ni janga la dunia ugonjwa wa Corona hadi pale watakapopata taarifa za kidiplomasia kuhusu uginjwa huo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la  Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo bungeni leo Jnanuari 30.

Ambapo Chumi amehoji serikali imejipangaje katika kudhibiti ugonjwa huo unaotokana na virusi vya corona ambavyo vinaonekana kuenea na kusambaa kwa kasi zaidi duniani.

Majaliwa akijibu swali hilo amesema kuwa kwa sasa Tanzania haina shida na Corona lakini wanachukua tahadhari kubwa hivyo wanafanya mawasiliano ya karibu na Ubalozi wa Tanzania nchini China.

Ambapo amesema wametafuta madaktari ambao wamekuwa wakitoa elimu kwa watanzania kuhusu ugonjwa huo.

Aidha Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya watu 4537, wameugua ugonjwa huo na watu 106 wamefariki dunia tangu ugonjwa huo uzuke chini China katika mji wa Wuhan.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad