Waziri wa Fedha Adaiwa Kulisababishia Taifa Hasara ya Tsh Milion 80 Kila Siku




Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (CHADEMA) amedai kila siku Taifa linateketeza Tsh. milioni 80 kulipa wakandarasi kutokana na Waziri Philip Mpango kushindwa kuruhusu Shirika la Nyumba (NHC), kumalizia miradi yake ya ujenzi wa nyumba

Miradi hiyo minne ukiwemo ule ya Morocco na Kawe, Jijini Dar es Salaam imekwama kwa maelezo kwamba, Waziri Mpango amekataa kutoa kibali cha kupata fedha ili kumalizia miradi hiyo kwa madai, Serikali imehamia Dodoma

Kutokana na hali hiyo, Serikali imelazimika kuwalipa wakandarasi wanne kila mmoja Tsh. milioni 20 kwa siku, wakisubiri uamuzi wa Waziri Mpango kumalizia ujenzi huo ili watu waanze kupanga ama kununua na kurejesha fedha hizo

Kutokana na hali hiyo, miradi hiyo imekwama na kusababisha kuwepo kwa hasara ambayo ingeweza kuepukika
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad