What a Big Surprise..Simba Amekufa na Utitiri Bandani..Mpira Hauna Adabu hata Kidogo.



✍️ Ulitegemea jana mashabiki wa Simba kushika tama kama wapo kilioni kwa zaidi ya nusu saaa?

✍️ Uzuri hili nililitambua mapema.  Nilifahamu mashabiki wa Simba watakwenda uwanjani na matokeo ndio maana walilowa.

✍️ Jana mchana niliwapa alama 3 Simba katika mchezo wa jana hususani suala la nidhamu ya mchezo. Yanga niliwapa alama 9. Nilifaham fika Simba wataidharau Yanga.

✍️ Baada ya bao la pili Simba walidhani wamemaliza. Utagundua Simba waliopoa mtoto mkali wakashindwa kumpa matumizi stahiki.

Kutongoza na kukubaliwa sio ishu, je unahudumia? Simba walishindwa kuhudumia mtoto mabaharia wamepita nae ndani ya dakika 3 tu

✍️ Balama a joy to watch. What screamer. Ule M'bao aliwahi kumtungua tena Manula akiwa na Alliance

✍️ Nilipoona hakuna Fraga nilikajua fika ujio wa Niyonzima eneo lile ukimchanganya na Balama Simba itavurugwa eneo hilo.

✍️ Juzi nilimsifia Niyonzima kurejea Yanga. Watu wakamkejeli. Niyonzima ameleta uhai mkubwa sana game ya jana

✍️ Eneo ambalo Simba walipoteana ni kiungo eneo ambalo wanasifika kwa ubora. Ukitazama goli walilofungwa ni uzembe katika eneo la kiungo (Muzamiru)

✍️ Goli alilosababisha Muzamiru leo aliwahi kusababisha tena mechi na Kenya Cecafa. Anapenda kugeuka bila tahadhari jambo ambalo ni hatari kwa viungo hatarishi.

✍️ Jana nilitabiri kuwa eneo la ulinzi la Yanga litaamua matokeo. Yondani na Sonso wamehakikisha Kagere anapiga penati tu.

✍️ Taironi aliifanya kazi yake kwa umakini sana wala sikutegemea. Tshishimbi ametakata sana leo. Mkwasa kweli masta. Ule muunganiko wa Banka, Makame na Tshishimbi balaa.

Kwa namna yanga ilivyopangwa jana imepangwa kiufundi kaisi kwamba natamani kumjua aliyemwamsha Mkwasa leo

Simba walicheza vizuri sana. Lakini walikosa utulivu wa kisaikolojia. Ile comeback iliwakata moto. Sub ya Kanda iliharibu mipango. Build up yao ilikuwa nzuri lakini Yanga walicheza kwa utulivu mkubwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad