Wizara ya Mambo ya Nje yasema haijapokea taarifa kuhusu Tanzania kuwekewa vikwazo na Marekan


Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Emmanuel Buhohela amesema kuwa hadi sasa haijapokea waraka wowote wa Kidplomasia kutoka nchini Marekani, kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zitawekewa vikwazo.


Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Emmanuel Buhohela
“Sisi kama Wizara mawasiliano yote huwa yanafanyika kwa Waraka maalumu wa Kidplomasia, ndio maana kuna Ubalozi kwahiyo kama kungekuwa na jambo lolote wangetueleza kwa kutumia njia hiyo, na hadi sasa hatujapata ujumbe wowote na hatuwezi kuzungumzia vitu ambavyo vinasemwa kwenye mitandao” Buhohela aliiambia EATV.

Hayo ni baada ya taarifa zilizosambaa zinazodai kwamba Serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwa na mpango wa kuziongeza Nchi nyingine 7, ikiwemo Tanzania kwenye orodha ya Nchi ambazo, Raia wake wamewekewa vikwazo vya kuingia nchini humo.

Source: EATV

By. Jacquiline Ngoya


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad