Wizi wa Betri za taa Barabarani Waibuka Moshi
0
January 17, 2020
Taa zinazotumia mwanga wa jua (sola) zilizowekwa katika barabara mbalimbali katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro zimeanza kuharibiwa na baadhi ya watu kwa kuiba betri na nyaya zake.
Mradi huo wa taa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya milioni 947 za kitanzania, ulilenga kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo na kumaliza vitendo vya wizi, uporaji na ubakaji nyakati za usiku.
Akizungumza na waandishi ya habari jana, Diwani wa Bomambuzi, Juma Raibu amesema hadi kufika januari 13, 2020 zilikuwa zimeibiwa betri zaidi ya tano pamoja na nyaya zake.
Amebainisha kuwa ufungaji wa taa moja ulighalimu zaidi ya milioni 3 za kitanzania, hivyo kuibiwa kwa betri hizo kumeisababishia halmashauri hiyo hasara ya mamilioni ya fedha.
Tags