Yanga Yaifunga Prison 2-0 Kombe la FA, Morrison na Yikpe Watupia



Timu ya Yanga SC imeshinda mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Jumapili, Januari 26, 2019.

Yanga ilipata bao  la kwanza katika dakika 10, kwa mkwaju wa penalti ya Morrison baada ya beki wa Prisons Michael Isamail kuunawa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo, Athuman Lazi kutoka Morogoro kuamua adhabu hiyo na bao la pili limefungwa na Yikpe dakika ya 63.

 

Ikicheza mbele ya mashabiki wachache waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga ilipata wakati mgumu kutokana na ushindani mkali ulionyeshwa na Prisons.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad