Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Mkoani Tanga, imezoea upinzani ambapo madiwani Nane wa CUF wamekihama Chama hiko na kujivua nafasi zao zote na kujiunga na CCM.
Uamauzi huo wameufanya katika mkutano wa ndani wa Katibu Mkuu wa CCM alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata wilaya ya Tanga mjini katika uwanja wa Mkwakwani jana tarehe 15 Januari, 2020.
Viongozi hao wameongozwa na Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Tanga Ndg. Bashiru Azizi na Naibu Meya wa jiji la Tanga Ndg. Haniu Ally kata ya Tangasisi, madiwani wengine ni Mswahili Njama Kata ya Chongoleani, Ndg. Said Alei Diwani Kata ya Masiwani na Habibu Mpa Diwani Kata ya Ngamiani Kati.
Wengine ni Ndg. Nassoro Salimu Diwani Kata ya Tongoni, Akida O. Akida Diwani Kata ya Ngamiani Kaskazini, Mwanaisha Abdala Diwani Viti Maalum Tarafa ya Chumbageni, Thurekha Mahadhi Diwani Viti Maalum Tarafa ya Ngamiani na Mke wa Mbunge wa CUF Tanga Mjini.
Licha ya viongoz hao, Makada wengine waliokihama Chama hiko wameongozwa na Bi. Hidaya Ahmed aliyekuwa Kampeni Meneja wa Jimbo la CUF.
Madiwani hao waliojiunga na CCM wameeleza sababu mbalimbali za kukihama Chama hiko, ikiwa ni pamoja na vyama vyao kukosa dira ya uongozi na kuelekea kupoteza uhalali wa kuomba ridhaa ya kuwaongoza Watanzania, hivyo wamerudi CCM kutoa mchango katika maendeleo makubwa yanayoendelea kufanyika chini ya umadhubuti wa CCM inayoongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Ndg. John pombe Joseph Magufuli.