Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kablwe, amesema mkopo ambao serikali ya Tanzania inaomba Benki ya Dunia ni kwa ajili ya kisiasa.
“Elimu ya watoto wa kike ni sehemu tu ya mkopo huo wa Shs. 1.5 trilioni,” aliandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.
Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini alisema katika mwaka wa Uchaguzi wa serikali iliyotapanya fedha kununua midege, inatafuta mkopo wa kujenga shule 1000.
Kiongozi huyo alisema mkopo huo ni sehemu ya kampeni.
Zitto aliandika ujumbe unaosomeka hivi”Mkopo ambao serikali ya Tanzania inaomna Benkinya Dunia ni mkopo wa kisiasa. Elimu ya watoto wa like ni sehemu tu ya mkopo huo wa Shs. 1.5 trilioni. Katika mwaka wa uchaguzi serikali iliyotapanya fedha kunumja midege, inatafuta mkopo wa kujenga shule 1000. Ni mkopo wa kampeni,”
Mkopo ambao Serikali ya Tanzania inaomba Benki ya Dunia ni mkopo wa kiSIASA. Elimu ya watoto wa kike ni sehemu tu ya mkopo huo wa Shs. 1.5 trilioni. Katika mwaka wa Uchaguzi Serikali iliyotapanya Fedha kununua midege, inatafuta mkopo wa kujenga Shule 1000. Ni mkopo wa kampeni— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) January 27, 2020