Heche Amrarua RC Gambo "Tangu Lini mtu Akisema Barabara ni Mbovu iwe Kuhujumu Uchumi?"



Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amemtolea povu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa kauli aliyoitoa ya udikteta .

“Wale wenye wasiwasi bado kuhusu sehemu nchi yetu imefikia waangalie upuuzi huu… Tunazama kwenye udikteta kwa haraka sana… Korea Kaskazini inaundwa Tanzania,”

Kiongozi huyo aliandika ujumbe huu katika ukurasa wake wa Twitter kuwa “Hivi kusema barabara ni mbovu ni kuhujumu uchumi?,” alihoji Heche.

Heche alisema unahujumu uchumi vipi kwa kusema ukweli? aibu kubwa kwa CCM.

Leo Gambo amegiza  polisi kumsaka aliyetuma picha katika mitandao ya kijamii kuonyesha ubovu wa miundombinu ya barabara ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Amesema kitendo hicho ni sawa na kuhujumu uchumi kwani watu hao wangeweza kutumia njia sahihi kuwasilisha taarifa hizo na kuzituma katika mitandao ya kijamii.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad