Wasira Amvaa Zitto Kabwe "Kuzuia Pesa sio Jibu"



Aliyekuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na Mbunge wa jimbo la Bunda  Stephen Wasira amemjibu kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyeiandikia barua Benki ya Dunia (WB) kuishawishi kutoipatia Tanzania fedha kwa ajili ya sekta ya elimu.


Ameongea hayo wakati akihojiwa leo Jumatatu Februari 10, 2020 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds,  Wasira amesema Zitto si mzalendo kunapokuwa na jambo lenye maslahi ya Taifa nchi kubwa kama Marekani huwa wanaweka tofauti zao pembeni na wanaungana.

"Nilimsikiliza Zitto wakati akizungumza na Watanzania walioko nje ya nchi, mmoja alimuuliza Zitto kuwa anasema Benki ya Dunia isitoe mkopo si utawauzima Watanzania wote? Alijibu Ilani ya CCM ilisema watoto wakipata mimba wasome, namwambia Zitto kuzuia pesa sio jibu, ili kuwasaidia wasichana wasipate mimba ni kutumia hizo pesa kujenga hostel na wachumba watakaa mbali sana kuwachumbia wasichana“ alisema Stephen Wasira.


Yupo Mtanzania mmoja anaitwa Salma alimuuliza Zitto swali hili, “lakini wewe (Zitto) sasa unataka benki isitoe mkopo, kwa kufanya hivi si unawaumiza Watanzania wengi zaidi kuliko kuwasaidia, inasaidia nini?”

Wasira amesema katika majibu yake Zitto amesema, “ilani (ya CCM)  ilisema wakipata mimba wasome.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad