Ado Shaibu afunguka kuhusu Lowasa, Sumaye kurudi CCM
0
February 13, 2020
Vyama vya upinzani vimetakiwa kuwa makini na kuwachuja wanasiasa wanaotoka chama tawala hasa wale waliowahi kuwa na madaraka na kushiriki kuwahujumu wapinzani na kuwaminya kwakuwa hawawezi kubadilika na kuwa wazuri kwa wapinzani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Uenezi wa Chama ACT - Wazalendo Ado Shaibu alipofanyiwa mahojiano na muungwana blog na kusema kuwa mtu kama Lowasa na Sumaye wameshachoka maisha ya kisiasa wameamua wachukue mkondo tu wakufanya maisha yao binafsi.
"Hama hama za wanasiasa kurudi kwenye chama cha CCM ni ishara ya kigeu geu na unafki, Sumaye alipoingia Chadema alijenga hoja ya kwamba aliona ndani ya CCM hakuna demokrasia na kuamua kujiunga CHADEMA ili kuujenga upinzani utakaokuja kuiondoa CCM madarakani' alisema Ado Shaibu.
"Sumaye alijenga hoja kuwa hata apewe trilioni 50 hawezi kurudi CCM na alieleza kuwa, aliweza kupitia misukosuko mingi ndani ya biashara zake na maisha yake, sasa anarudi CCM na kusema CCM ni nyumbani inaonyesha mwanasiasa kigeugeu" alisema Ado
Ado alisema hilo liwe funzo kwa wapinzani kwa wanaotoka CCM kwenda upinzani wanatakiwa kumulikwa kwa umakini kwakuwa lipo kundi la kwanza la wana CCM ni kweli wapiganaji wamekosa haki wanakuja upinzani kuidai haki hiyo kwenye mageuzi, hao wakaribishwe.
Tags