Akiwa Marekani Roma Aweka Historia Mpya
0
February 28, 2020
Wakati bado yupo nchini Marekani akifanya shughuli zake binafsi MwanaHipHop Roma Mkatoliki, ameweka rekodi mpya ya kushika namba 1 kati ya wasanii 10 wa HipHop Afrika Mashariki wenye wafuasi wengi katika mtandao wa YouTube.
Akitoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya Instagram na Twitter, Roma Mkatoliki anaongoza kwa kuwa na wafuasi 265k.
Orodha ya wasanii wengine ambapo namba 2 imekwenda kwa Nyashinski 252k, Kenya 3. Darassa 240k, Tanzania 4. Khaligraph Jones 220k, Kenya 5. King Kaka 219k, Kenya 6. Nay Wa Mitego 180, Tanzania 7. Dogo Janja 161, Tanzania 8. Octopizzo 143k Kenya 9. Proffesor Jay 119k Tanzania 10. Young Killer 91k Tanzania.
Kwa upande wa Roma Mkatoliki Mwenyewe amesema "HipHop na Rap ni muziki unaopendwa sana na watu na una mashabiki wengi sana, sina uhakika na hili,kwamba kwenye "Digital Platforms" hatuna wafuasi wengi ukilinganisha na aina nyingine za muziki, kwahiyo mimi kuwapata wafuasi 265K na kuwa namba 1 Afrika Mashariki na Kati, haikuwa rahisi hata kidogo, hii ni baraka"
Tags