Ally Mayai Tembele: Yanga inajidanganya yenyewe


Niliwahi kuandika Yanga inajidanganya yenyewe na kuishi kwa kivuli cha timu kubwa na kudhani labda dunia imesimama kumbe dunia inakimbia kwa kasi mno.
Nilisema Yanga imedumaa na siku ikija kushtuka na kutaka kwenda sambamba na dunia itakuta tayari Simba imeliteka soko lote la Uchumi wa soka nchini.
Nilitoa mfano wa Juventus, Porto, Buyen Munich, Mazembe, Gor na Horoya kwamba timu hizi tayari zimejimilikisha Uchumi wa soka wa nchi zao. Leo hakuna mchezaji wa Kijerumani asiyetamani kuchezea Buyern.
Au mchezaji anayezaliwa Italy ndoto yake kuu ni kucheza Juventus. Na tunakoelekea na Tanzania hali ndiko inakoelekea. Simba inajimilikisha kwa kasi ya ajabu uchumi wa soka. Yanga wamebaki kujivunia juzi na jana na sio leo na kibaya zaidi sioni kesho yao.
Kama Kuna kosa kubwa kuliko yote linafanyika ni pale wanapobeza mafanikio ya Simba na kuwaponda mwekezaji wa Mohamed Dewji. Wamekuwa wakitafuta mapungufu machache yaliyopo Simba na kuyafanya ndio agenda yao.

Wamesahau kabisa kuitazama timu yao na mkwamo uliopo wameamua kuitukuza Simba na kuitaja aidha kwa mapungufu au kuwabeza Kama watani. Wanasahau hapa wao wenyewe ndio wanaikuza brand ya Simba na kuifanya kutajwa mno midomoni kila siku.
Leo Yanga hawana hata Jambo Moja wanaloweza kupambana na Simba aidha ndani au nje ya Uwanja. Wamezidiwa kila udara na itawachukua muda mrefu mno kufikia Simba ilipo Sasa.
Yanga hawajakubali bado kubadilisha mfumo wao wa uendeshaji wa timu kutoka wa kizamani na wa kiholela kuja kwenye mfumo wa kisasa na hii inasababishwa na walaghai tena wezi wa jasho la wachezaji kuwahadaa ni timu ya wananchi na wasikubali mwekezaji kwa kuwa timu itakuwa si Mali yao Tena. Huu ndio uongo uliotukuka wanaoutumia walaghai kuendelea kujinufaisha kupitia klabu hii.

Embu tujiulize nyie wapenzi na mashabiki wa Yanga lini mlinunuliwa hata soda na klabu zaidi ya nyie kuchangishwa? Sasa hicho mnachoaminishwa mtakipoteza ni kipi? Wanaoogopa kupoteza ni wale akina fulani ambao maisha yao yanategemea timu kuendelea kuishi mjini. Na hawa huwa hawachangii zaidi ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha ili wazizungukie mlango wa nyuma wakaziibe. Sisi tunaochanga Wala hatuna Cha kupoteza
Nahisi kwenye miaka ya sitini ni kweli mashabiki wa Yanga labda walikuwa wengi kuliko wa Simba na mkabweteka na mkasahau watu wanazaliwa na kufa. Nimebahatika kwenda karibu viwanja vyote vya soka nchini. Nawahakikishia kwa  sasa Simba Ina mashabiki wengi kuliko timu zote nchini.

ENDELEENI KULALA MKIAMKA TAYARI JUA LITAKUWA LINAZAMA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad