Askari POLISI Wamchoma Singe Mwenyekiti wa Kitongoji


Mwenyekiti wa Ulinzi wa Kijiji cha Peramiho A ambaye pia ni Mwenyekiti Kitongoji cha Mtakuja, Pastorius Mbuya amejeruhiwa kwa kipigo cha Askari Polisi

Inaelezwa Askari hao walichukizwa na Mwenyekiti huyo kumpigia simu Mkuu wao wa kazi na kuwagongea usiku wakati Kituo cha Polisi kimefungwa

Mbuya alienda Kituoni hapo saa sita usiku kushughulikia suala la Mwanafunzi na ndipo Askari walikataa kumshughulikia baada ya kukuta Kituo kimefungwa hivyo kitendo cha kugonga kiliwachukiza Askari

Kwa mujibu wa Kituo cha habari cha ITV, Dereva wa bodaboda, aliyempeleka Mbuya Kituo hapo anasema alishuhudia Askari wakimtukana Mbuya kabla ya kumpiga na kumchoma singe ya bunduki mguuni na mkononi

Aidha, akizungumza kwa simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, ACP Simon Marwa amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko kwenye uchunguzi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad