Baada tu ya taarifa kusambaa kuhusu tukio kubwa lililoukumba mji wa Moshi na waumini wa kanisa la Inuka Uangaze, kufuatia vifo vya watu 20 waliokuwa wakigombea kupakwa mafuta ya upako na Mtume Boniface Mwamposa, Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo, Askofu Paul Bendera alifanya mamombi maalum kwa ajili ya kumuombea kiongozi mwenzake wa kiroho, Mtume Mwamposa ili awe na roho ya ustahimilifu.
Askofu Bendera aliwaombea marehemu na majeruhi wote wa ajali hiyo pamoja na kuliombea rehema taifa ili kuondoa chuki dhidi ya kanisa na kuleta amani miongoni mwa wananchi na waumini wote.
Askofu Bendera ambaye amekuwa na maono makubwa, na hili limejidhihirisha siku moja baadaye baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati akituma salam za rambirambi zilizosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira wakati wa kuaga miili ya marehemu hao, Rais alisisitiza makanisa hayo yasifungwe badala yake yendelee na huduma za dini huku akiwaomba kuzifanyia kazi changamoto ndogondogo za kibinadamu.
Ikumbukwe kuwa, Septemba 9, 2015, Askofu Bendera aliwahi kumtabiria ushindi mkubwa rais wa sasa, Dkt. John Magufuli na baada ya uchaguzi maono yake yalitimia na Magufuli akawa rais wa Tanzania.